Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 14:25

WFP yasema msaada wa chakula unahitajika pembe ya Afrika


Mama akiwa na mtoto wake mwenye utapiamlo kwenye hospitali ya Banadir mjini Mogadishu nchini Somalia, Julai 7, 2011
Mama akiwa na mtoto wake mwenye utapiamlo kwenye hospitali ya Banadir mjini Mogadishu nchini Somalia, Julai 7, 2011

Shirika la chakula duniani-WFP, linasema linatarajia watu milioni 10 watakuwa wanahitaji msaada wa chakula, wakati ukame mbaya kuwahi kutokea katika miongo kadhaa unaendelea kulikumba eneo la pembe ya Afrika.

Ukame upo kwenye maeneo matatu ya nchi ya Kenya, Somalia na Ethiopia. Ukame huo umesababisha uhamaji mkubwa wa raia waliokumbwa na njaa na kusababisha kuwepo na kambi kubwa ya wakimbizi duniani.

Kambi ya Dadaab iliyopo kaskazini mashariki mwa Kenya, ilijengwa ili kuhudumia wakimbizi 90,000, hivi sasa inawakimbizi zaidi ya 380,000 wa kisomali, na mamia zaidi ya wakimbizi wanamiminika kila siku.

Kambi hiyo ilitembelewa Jumapili na Antonio Guterres, mkuu wa shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa-UNHCR. Baadae aliwaambia waandishi wa habari kwamba msaada mkubwa unahitajika kupambana na janga baya la kibinadamu duniani.

Mashirika ya kimataifa yanakabiliwa na wakati mgumu wa kutoa msaada kwa wale ambao wamebaki nchini Somalia, ambayo ina ukosefu wa serikali inayofanya kazi na eneo lake kubwa linadhibitiwa na kundi la uasi la Al-shabab.




XS
SM
MD
LG