Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Mei 14, 2021 Local time: 04:02

Westgate Mall yakombolewa na majeshi ya Kenya


Polisi wa Kenya wakiwa Westgate Mall
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta Jumanne jioni ametangaza kuwa operesheni za kijeshi dhidi ya magaidi zimemalizika katika maduka ya kifahari ya Westgate Mall jijini Nairobi.

Rais Kenyatta alisema Kenya imewaaibisha washambuliaji hao, kuwauwa magaidi watano na kuwakamata wengine 11 ambao wamezuiliwa. Alisema takriban watu 61 wamethibitishwa kufa tangu magaidi hao walipovamia maduka hayo Jumamosi.

Msako huo uliingia siku ya nne leo Jumanne huku jeshi la ulinzi la Kenya KDF likisema linaudhibiti wa maduka hayo. Watu 240 walijeruhiwa kwenye shambulizi hilo.

Rais huyo wa Kenya pia ametangaza siku tatu za maombolezi ya kitaifa kufuataia shambulizi hilo.

Ona maoni (1)

mjadala huu umefungwa
XS
SM
MD
LG