Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Juni 16, 2024 Local time: 15:18

Waziri wa zamani wa Msumbiji ahukumiwa kifungo cha miaka 16 jela kwa makosa ya ufisadi


Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku kuu ya jeshi katika mji wa Pemba, Septemba 25, 2021. Picha ya Reuters
Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku kuu ya jeshi katika mji wa Pemba, Septemba 25, 2021. Picha ya Reuters

Msumbiji Alhamisi imemuhukumu waziri wa zamani kifungo cha miaka 16 jela kwa makosa ya ufisadi, ikiwa ni hukumu kali kwa nchi ambayo bado inakabiliana na athari za kashfa tofauti ya ubadhirifu.

Maria Helena Taipo, mwenye umri wa miaka 60, mwanachama wa chama tawala cha FRELIMO ambaye aliongoza wizara ya kazi kuanzia mwaka wa 2005 hadi 2014, anashutumiwa kwa ubadhirifu wa milioni 113 pesa za Msumbiji, sawa na dola milioni 1.7, ambazo ni fedha za serikali kwa kujenga nyumba yake na matumzi mengine ya kibinafsi.

Maafisa wengine wanane wa serikali walipewa hukumu iliyo kati ya miaka 12 na 16 jela katika kesi hiyo.

Jaji wa Maputo Evandra Uamasse amesema wakati wa kutoa hukumu hiyo, “wakiendeshwa na tamaa ya kupata faida kiurahisi”, washtakiwa walipoteza imani ya umma.

“Mahakama inatakiwa kuwa na msimamo wa uthabiti na ukali ili kuzuia tabia ya aina hii isirudiwe tena,” Uamasse amesema.

Wakili wa Taipo Inacio Matsinhe amesema mteja wake atakataa rufaa dhidi ya uamzi huo.

XS
SM
MD
LG