Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Oktoba 10, 2024 Local time: 20:07

Waziri wa zamani na mfanyabiashara nchini Tunisia wawekwa kizuizini kwa tuhuma za ufisadi


Waziri wa zamani wa uchukuzi waTunisia Abderrahim Zouari
Waziri wa zamani wa uchukuzi waTunisia Abderrahim Zouari

Tunisia imewakamata waziri wa zamani Abderrahim Zouari na mfanyabiashara Marouane Mabrouk, ambaye alikuwa mkwe wa rais wa zamani Zine El Abidine Ben Ali, kwa tuhuma za ufisadi, ripoti za vyombo vya habari zilisema Jumatano.

Tunisia imewakamata waziri wa zamani Abderrahim Zouari na mfanyabiashara Marouane Mabrouk, ambaye alikuwa mkwe wa rais wa zamani Zine El Abidine Ben Ali, kwa tuhuma za ufisadi, ripoti za vyombo vya habari zilisema Jumatano.

Watuhumiwa wote wawili waliwekwa chini ya ulinzi Jumanne kwa siku tano, kipindi ambacho kinaweza kurejelewa, msemaji wa mahakama ya mwanzo ya Tunis, Mohamed Zitouna, alinukuliwa akisema.

Walikamatwa kwa tuhuma za ufisadi huku kukiwa na uchunguzi wa kitaifa kuhusu faida iliyopatikana kwa njia zisizo halali chini ya utawala wa Ben Ali, ambaye aliondolewa madarakani katika mapinduzi ya Tunisia ya mwaka 2011 na kufariki mwaka 2019.

Zouari, ambaye alikuwa waziri wa uchukuzi kuanzia mwaka 2004 hadi 2011, anashukiwa kutumia nafasi hiyo kwa manufaa yake binafsi, alisema Zitouna. Kufuatia kuondolewa kwa Ben Ali mwaka 2011, serikali iliyachukua makampuni kadhaa, yakiwemo ya Mabrouk.

Lakini watendaji wengi na wamiliki walibakia kuwa wakuu wa makampuni hayo huku serikali ikifanya kazi kama mbia na mkaguzi.

Mabrouk anaongoza baadhi ya biashara kubwa sana Tunisia ikiwemo za mlolongo wa bidhaa za reja reja za Monoprix, kampuni ya simu ya Orange Tunisie na Benki ya Kimataifa ya Arab International Bank of Tunisia.

Mwaka 2022, Rais wa Tunisia Kais Saied alianzisha mradi ambapo wahalifu hulipa adhabu kubwa kwa baadhi ya uhalifu fulani wa kiuchumi badala ya kushtakiwa, katika kuongeza pato la serikali na kupunguza deni la taifa. Chanzo cha habari hii ni shiika la habari la AFP

Forum

XS
SM
MD
LG