Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Julai 14, 2024 Local time: 22:45

Waziri wa Usafiri wa Ubelgiji ajiuzulu


Waziri wa Usafiri wa Ubelgiji, Jacqueline Galant akiongea na waandishi wa habari mjini Brussels, April 15, 2016.
Waziri wa Usafiri wa Ubelgiji, Jacqueline Galant akiongea na waandishi wa habari mjini Brussels, April 15, 2016.

Waziri wa usafiri wa Ubelgiji, Jacqueline Galant, amejiuzulu leo Ijumaa baada ya kushutumiwa kupuuza ripoti ya Umoja wa Ulaya ya mapungufu ya usalama kwenye viwanja vya ndege nchini humo.

Galant amekuwa kiini cha ukosoaji baada ya ripoti ya siri ya Umoja wa Ulaya kusikitishwa na hali ya usalama kwenye viwanja vya ndege vya Ubelgiji, kuvuja kwenye vyombo vya habari kufuatia shambulizi la mabomu la Machi 22 ambalo liliuwa watu 32 wakiwemo 16 kwenye uwanja wa ndege wa kitaifa na kituo cha reli.

Kundi la Islamic State lilidai kuhusika na mashambulizi.

XS
SM
MD
LG