Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 03, 2023 Local time: 07:09

Waziri wa ulinzi wa Marekani awasili Libya


Waziri wa ulinzi wa Marekani Leone Paneta

Atakuwa Libya katika ziara ya kutathmini hali ilivyo baada ya mapinduzi ya kumuondoa Ghadafi


Waziri wa ulinzi wa Marekani Leone Paneta amewasili libya kwa ajili ya mazungumzo na Serikali ya mpito ya Libya , ziara ambayo ni ya kwanza kwa mkuu wa usalama wa Marekani nchini humo.


Safari hiyo ya Jumamosi imekuja baada ya Marekani kuondoa vikwazo vingi vya kiuchumi dhidi ya Libya katika juhudi za kupunguza mzozo wa kifedha nchini humo.

Panetta atakutana na waziri mkuu wa Libya Abdurrahim el- Keib na waziri wa ulinzi wa Libya Osama al- Juwali .


Awali Paneta aliwaambia waandishi wa habari kwamba ziara yake itamwezesha kutathmini hali ilivyo mara baada ya mapinduzi huko Libya na kumruhusu kutoa heshima kwa wale waliosaidia kumuondoa Ghadafi.


Jana Marekani iliachia zaidi ya dola bilioni 30 za mali ya serikali ya Libya ikifuatiwa na hatua kama hiyo ya baraza la usalama la umoja wa mataifa.

XS
SM
MD
LG