Nchi hiyo, ambayo ni maarufu kwa utalii na moja wapo ya mataifa imara zaidi barani Afrika, hufanya uchaguzi kila baada ya miaka mitano, na wa mwisho ulifanyika mnamo 2014.
Kisheria, Wananchi wa Mauritius wana kati ya siku 30 hadi 150 kushiriki uchaguzi baada ya waziri mkuu kuvunja bunge.
Jugnauth, mwenye umri wa miaka 57, ambaye pia ni waziri wa Fedha atawania muhula mwingine kama kiongozi wa chama kinachotawala cha MSM.
Amehudumu kama Waziri Mkuu tangu mwaka 2017 wakati alipochukua madaraka kutoka kwa baba yake, Anerood Jugnauth.
-Imetayarishwa na Mwandishi wetu Washington DC