Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Februari 11, 2025 Local time: 01:45

Waziri wa mambo ya nje wa Zambia ajiuzulu


Waziri wa mambo ya nje wa Zambia Stanley Kakubo (kulia) akiwa Washington, December 13, 2022. Picha na REUTERS/Evelyn Hockstein/Pool
Waziri wa mambo ya nje wa Zambia Stanley Kakubo (kulia) akiwa Washington, December 13, 2022. Picha na REUTERS/Evelyn Hockstein/Pool

Waziri wa mambo ya nje wa Zambia Stanley Kakubo amejiuzulu siku ya Jumanne, ofisi ya rais imesema, baada ya saa kadhaa za kukumbwa na kizaaza kwenye mitandao ya kijamii kwa madai ya kufanya makubaliano na mfanyabiashara wa Kichina.

Kakubo, mwenye umri wa miaka 43, alikuwa waziri wa mambo ya nje tangu mwezi Septemba 2021, amesema katika barua yake anaacha kazi kwa sababu ya “tuhuma mbaya kuhusiana na shughuli za kibiashara”

Awali, picha za video zilisambaa haraka kwenye akaunti za mitandao ya kijamii huko Zambia, zikiwaonyesha watu wawili wakihesabu pesa zilizokuwa zimepangwa mezani.

Picha ya ujumbe ulioandikwa kwa mkono, ukionyesha kuwa umeandikwa Julai 8, 2022, uliwekwa mtandaoni.

Ujumbe huo uliitaja kampuni ya madini ya Kichina na kampuni ya madini ya Zambia na ukisema kuwa wame “wamebadilishana dola 100,000”

Hata hivyo majina ya Kakubo na Zang hayakuwemo kwenye ujumbe huo, taarifa hizo hazikuweza kupata ufafanuzi wa haraka

Chanzo cha habari hii ni Shirika la habari la AFP

Forum

XS
SM
MD
LG