Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Mei 04, 2024 Local time: 03:24

Waziri wa mambo ya nje wa Russia, kutembelea China


Waziri wa mambo ya nje wa Russia, Sergei Lavrov, atatembelea China, Jumatatu na Jumanne kujadili vita vya Ukraine, na kuimarisha ushirikiano kati ya Moscow na Beijing.

Waziri wa mambo ya nje wa Russia, Sergei Lavrov, atatembelea China, Jumatatu na Jumanne kujadili vita vya Ukraine, na kuimarisha ushirikiano kati ya Moscow na Beijing.

Mazungumzo ya Lavrov na waziri wa mambo ya nje wa China, Wang Yi, ambaye alitoa mwaliko kwa waziri wa Russia, yatajumuisha ushirikiano wa pamoja na masuala muhimu kama vile mgogoro nchini Ukraine, na Asia-Pacific, imesema wizara ya mambo ya nje ya Russia imesema.

Reuters iliripoti mwezi uliopita kwamba rais wa Russia, Vladimir Putin atasafiri kwenda China, mwezi Mei, kwa mazungumzo na rais wa China, Xi Jinping, katika kile kinachoweza kuwa safari ya kwanza ya mkuu wa Kremlin, nje ya nchi katika muhula wake mpya wa urais.

China na Russia zilitangaza ushirikiano usio na kikomo Februari 2022 wakati rais Putin, alipoitembelea Beijing, siku chache kabla ya kupeleka maelfu ya wanajeshi nchini Ukraine, na kuanzisha vita vilivyosababisha vifo vingi zaidi barani Ulaya toka vita vya pili vya Dunia.

Forum

XS
SM
MD
LG