Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 22, 2024 Local time: 18:06

Waziri wa mambo ya nje wa Russia, atembelea Mauritania


Waziri wa mambo ya nje wa Russia, Sergei Lavrov, kushoto akisalimiana na waziri wa mambo ya nje wa Mauritania, Mohamed Salem Ould Merzoug.
Waziri wa mambo ya nje wa Russia, Sergei Lavrov, kushoto akisalimiana na waziri wa mambo ya nje wa Mauritania, Mohamed Salem Ould Merzoug.

Waziri wa mambo ya nje wa Russia, Sergei Lavrov, Jumatano amejitolea kutoa msaada kwa Mauritania katika vita dhidi ya vitendo vya jihadi  huko  Sahel, akisema anaheshimu msimamo wa  nchi hiyo katika vita vya Ukraine. 

Ziara ya Lavrov mjini Nouakchott ni sehemu ya juhudi kubwa za kidiplomasia za Russia, barani Afrika, ambazo zimezidisha ushindani wa kimkakati baina ya mataifa yenye nguvu.

Siku ya Jumanne, aliitembelea Mali, ambako Russia, imekuwa mshirika mkuu wa utawala wa kijeshi.

Akiwa huko, aliahidi kuzisaidia nchi za Sahel na nchi za Ghuba ya Guinea katika vita dhidi ya harakati za kijihadi, na akadokeza kuongezeka kwa ushiriki wao katika bara hilo.

Mauritania ni nchi muhimu kati ya eneo la Maghreb na Afrika ya Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Harakati za msimamo mkali zimeenea katika nchi za Sahel za Mali, Burkina Faso na Niger na sasa zinatishia Ghuba ya Guinea upande wa kusini kabisa, ingawa Mauritania haijashuhudia shambulio lolote toka 2011.

Nchi hiyo kubwa yenye watu milioni 4.5 ilipiga kura Machi 2022 kuunga mkono azimio la Umoja wa Mataifa linaloitaka Russia kusitisha mara moja operesheni zake za kijeshi nchini Ukraine.

Nchi nyingi za Kiafrika hazikushiriki au hazikupiga kura kabisa.

Mwezi Oktoba, Mauritania ilipigia kura azimio dhidi ya kujiingiza imabavu kwa Russia katika mikoa minne ya Ukraine.

Lakini Novemba ilijiweka kando katika kura ya fidia ya vita ambayo Russia inapaswa kulipa kwa Ukraine.

Lavrov alisema nchi yake ina heshima kwa sera thabiti ya Mauritania ya kutoegemea upande wowote, na hilo kalikuzuia nchi hiuo kushughulikia kikamilifu matatizo ya kikanda.

Lavrov alipokelewa na Rais wa Mauritania Mohamed Ould Cheikh El Ghazouani, shirika la habari la taifa liliripoti.

XS
SM
MD
LG