Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Februari 16, 2025 Local time: 10:45

Waziri wa mambo ya nje wa Palestina aishutumu Israel kwa ubaguzi wa rangi


Waziri wa mambo ya nje wa Palestina Riyad al-Maliki, alipokuwa katika mkutano na waandishi habari huko Athens on Februari 15, 2024. Photo by Aris MESSINIS / AFP
Waziri wa mambo ya nje wa Palestina Riyad al-Maliki, alipokuwa katika mkutano na waandishi habari huko Athens on Februari 15, 2024. Photo by Aris MESSINIS / AFP

Waziri wa mambo ya nje wa Palestina Riyad al-Maliki, Jumatatu ameishitumu Israel kwa ubaguzi wa rangi wakati akiitaka mahakama kuu ya Umoja wa Mataifa kuutangaza ukaliaji wa Israel katika aridhi ya taifa la Wapalestina kuwa ni kinyume cha sheria za kimataifa.

Tuhuma hizo zimetolewa mwanzoni mwa kikao cha kihistoria kuanza kuskiliza uhalali wa Israel kuikalia ardhi inayopiganiwa kwa ajili ya taifa la Wapelstina kwa miaka 57.

Kesi hiyo inafanyika wakati wa kuendelea kwa vita kati ya Israel na Hamas, ambayo mara moja imekuwa sulala msingi kwa siku hiyo – pamoja na kuwa kesi hiyo inakusudia kuzingatia udhibiti wa Israeli usio na kikomo katika maeneo inayoyakalia ya Ukingo wa Magharibi , Ukanda wa Gaza na Jerusalem ya Mashariki iliyovamiwa.

Waziri wa mambo ya nje wa Palestina amesema anasimama mbele ya Mahakama ya Sheria za Kimataifa “wakati Wapalestina million 2.3 wa Gaza, nusu yao wakiwa watoto wamezunguukwa na kupigwa mabomu, kuuawa na kujeruhiwa, wakiwa na njaa na kupoteza makazi.

“ Zaidi ya Wapelestina milioni 3.5 walioko Ukingo wa Magharibi, ikiwemo Jerusalemu, wanakabiliwa na ukoloni kwenye ardhi yao na ghasia za ubaguzi wa rangi zinazoiwezesha,” aliongeza kusema al-Maliki.

Kikao hicho kinachotarajiwa kudumu kwa siku sita, kinafuatia ombi la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa la kutoa maoni yasiyofungamana na sheria kuhusu sera za Israel katika maeneo yanayokaliwa kimabavu. Huenda majaji watachukua miezi kadhaa kutoa maoni

Wapalestina wanadai kwamba, kwa Israel kunyakua sehemu kubwa ya aridhi inayokaliwa kwa mabavu, imekiuka marufuku kwenye ardhi iliyoteka na haki ya Wapalestina ya kujitawala, na kuweka mfumo wa ubaguzi na ubaguzi wa rangi.

Forum

XS
SM
MD
LG