Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Septemba 10, 2024 Local time: 11:34

Waziri wa mambo ya nje wa Jordan, ahitimisha ziara ya Iran


Waziri wa mambo ya nje wa Jordan, Ayman Safadi
Waziri wa mambo ya nje wa Jordan, Ayman Safadi

Waziri wa Mambo ya Nje wa Jordan, Ayman Safadi, amehitimisha ziara yake ya nadra ya Iran Jumapili, kwa kutoa mwito wa kukomesha kuongezeka kwa ghasia ili ukanda huo uwe na amani, usalama na utulivu.

Ziara ya Safadi, nchini Iran inafuatia kuendelea kwa mawasiliano ya kidiplomasia kati ya Marekani na washirika wake ikiwemo Ufaransa, Uingereza, Italia na Misri kwa ajili ya kuzuia ongezeko zaidi la mvutano wa kikanda kufuatia mauaji ya kiongozi wa Hamas, Ismail Haniyeh mjini Tehran.

Televisheni ya taifa ya Iran, imeripoti kwamba katika mkutano na Safadi, Rais wa Iran, Masoud Pezeshkian, amesema mauaji ya Haniyeh ni kosa kubwa la utawala wa Israel, ambalo halitapita bila kujibiwa.

Iran na Jordan zinaboresha uhusiano wao kufuatia mvutano wa karibuni baina yao.

Forum

XS
SM
MD
LG