Ziara yake inafanyika wakati maafisa wa Marekani wanataka kuiona China ikichukuwa njia bora wakati vita vya Israel na wanamgambo wa Hamas na huku Russia, ikiendelea na vita vyake dhidi ya Ukraine.
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Antony Blinken, atakuwa mwenyeji wa waziri Wang, hapo Oktoba 26 mpaka 28.
Mshauri wa usalama wa kitaifa wa White House, Jake Sullivan, pia atafanya mazungumzo na waziri Wang, kwa mujibu wa maelezo ya maafisa wawili wa ngazi ya juu wa utawala.
Sullivan alifanya mazungumzo na Wang huko Malta, Septemba 16 na17 kufuatia mikutano yao Vienna, mwezi Mei 10-11
Forum