Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 20, 2024 Local time: 12:46

Waziri wa fedha wa Marekani asisitiza umuhimu wa kuimarisha biashara kati ya Marekani na Korea Kusini


Waziri wa fedha wa Marekani Janet Yellen akuwa kwenye mkutani wa G20, mjini Bali,Indonesia.
Waziri wa fedha wa Marekani Janet Yellen akuwa kwenye mkutani wa G20, mjini Bali,Indonesia.

Waziri wa fedha wa Marekani Janet Yellen amesema kwamba Marekani na Korea kusini wanahitaji kuimarisha uhusiano wao wa kibiashara.

Yelln amesema kwamba hatua hiyo ni ili kuzuia kushirikiana na mataifa yanayotumia uwezo wao kuhujumu uchumi, wakati akiitaja China kwa jina.

//Hatuwezi kukubali mataifa kama China kutumia nafasi yao ya kibiashara kwenye teknolojia au bidhaa nyingine kuvuruga uchumi wetu kwa kutumia ushawishi wa kisiasa na kieneo.//

Waziri Yellen anatarajiwa kutoa hotuba kwenye kiwanda cha kampuni ya LG Corp kilichoko Korea kusini, ambayo Aprili lilitangaza mpango wa kutengeneza kiwanda cha kutengeneza betri kwa dhamani ya dola bilioni 1.4 kwenye mji wa Queen Creek, Arizona.

Yellen anawakilisha Marekani kwenye kundi la mawaziri wa fedha kutoka kundi la G20 kwenye mji wa kifahari wa Bali, Indonesia. Wakati akielekea huko alipitia Tokyo, Japan na mjini Seoul, Korea kusini. Hata hivyo hakuzuru China ingawa alifanya mawasiliano ya simu na naibu waziri mkuu wa taifa hilo mwanzoni mwa mwezi huu.

XS
SM
MD
LG