Yellen pia alisema pembeni ya mkutano wa mawaziri wa fedha wa nchi za G20 nchini India, atakanusha ukosoaji kuwa kuna malumbano kati ya misaada kwa Ukraine na mataifa yanayoendelea.
“Kukomesha vita hivi kwanza kabisa ni jambo la kimaadili,” aliwaambia waandishi wa habari mjini Gandhinagar.
“Lakini ni jambo bora zaidi tunaweza kufanya kwa uchumi wa dunia,” aliongeza.
Yellen pia alisisitiza juhudi za kukabiliana na tatizo sugu la madeni lyanayoyakabili mataifa yenye uchumi mdogo, mageuzi ya benki na makubaliano ya ushuru wa kimataifa, na akaonya kuwa ni “mapema”kuzungumzia juu ya kuondoa ushuru kwa China.
Forum