Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Oktoba 07, 2024 Local time: 21:27

Waziri wa fedha wa Marekani akutana na Spika Pelosi


Spika wa Baraza la Wawakilishi la Marekani, Nancy Pelosi, akiwa na kiongozi wa waliowachache Sen. Chuck Schumer, baada ya kukutana na waziri wa fedha wa Marekani, Steve Mnuchin Septemba, 30.
Spika wa Baraza la Wawakilishi la Marekani, Nancy Pelosi, akiwa na kiongozi wa waliowachache Sen. Chuck Schumer, baada ya kukutana na waziri wa fedha wa Marekani, Steve Mnuchin Septemba, 30.

Waziri wa fedha wa Marekani, Steven Mnuchin, na Spika wa Baraza la Wawakilishi Nancy Pelosi, walikutana Jumatano, ili kufikia muafaka juu ya msaada wa fedha kwa raia wa Marekani.

Fedha hizo ni kwa ajili ya kusaidia walioathiriwa na janga la virusi vya Corona, kabla ya bunge la Marekani kusitisha vikao vyake na kwenda kwenye kampeni za uchaguzi wa Novemba 3.

Wawili hao walikutana kujadili kwa kina yaliomo ndani ya muswada wa sheria ambao utatoa pesa zaidi kwa familia za Wamarekani, na Wafanyabiashara.

Fedha zitalenga mamillioni ya Wamarekani waliopoteza ajira, kutoa msaada wa fedha kwa majimbo na serekali za wilaya, pamoja na kulinda biashara zisifilisike.

Tofauti ilioonekana kwenye majadiliano hayo ni kuhusu kiwango cha msaada wenyewe.

Baraza la wawakilishi linalodhibitiwa na Wademocrats linajiaanda kupitisha msaada wa dola trillioni 2.2, ambao unapingwa na Warepublican.

Waziri Mnuchin ambaye anamuwakilisha rais Trump, ameiambia televijeni ya CNBC kwamba pendekezo la White House ni dola trillioni 1.5

Spika Pelosi ameiambia televijeni ya MSNBC kwamba ana matumaini ya kupatikana mkataba licha ya kuwa Wademocrats na Warepublican wanatofautiana kuhusu kiwango cha pesa ambacho kinapaswa kutolewa.

XS
SM
MD
LG