Ziara hiyo hata hivyo imekemewa vikali na China. Waziri huyo wa Uingereza Greg Hands atakuwa mmoja wa viongozi katika mazungumzo hayo ya kila mwaka, huku pia akitarajiwa kukutana na rais wa kisiwa hicho, Tsai Ing-wen wakati wa ziara hiyo ya siku mbili.
Taarifa zimeongeza kusema kwamba, sawa na Taiwan, Uingereza inazingatia sheria za soko huru la kimataifa. Msemaji kutoka kwenye ofisi ya kibalozi za Uingereza nchini Taiwan ameliambia shirika la habari la AFP kwamba shughuli rasmi za Hands zitaanza Jumanne.
Taiwan katika miezi ya karibuni imepokea wageni mashuhuri wa kimataifa, miongoni mwao akiwa spika wa bunge la Marekani Nancy Pelosi, aliyezua malalamiko makali kutoka Beijing. China imekuwa ikidai kukimiliki kisiwa hicho kinachojitawala kidemokrasia, wakati ikitishia kukichukua kwa nguvu ikiwezekana.