Nafasi ya Sarr itachukuliwa na Marie Khemesse Ngom Ndiaye, mkurugenzi mkuu wa wizara ya afya, kwa mujibu wa amri hiyo ya serikali.
Maafisa wanasema hitilafu ya umeme ndio ilisababisha moto kuzuka Jumatano jioni na kuua watoto hao wachanga katika hospitali ya mji wa magharibi mwa Senegal wa Tivaouane.
Rais Macky Sall ametoa taarifa ya msiba huo kwenye Twitter na kutangaza siku tatu za maambolezo ya kitaifa.
Meya wa mji wa Tivaouane Demba Diop amesema moto huo ulisababishwa na hitilafu ya umeme na ulisambaa kwa haraka sana.
Amekanusha madai ya ndugu wa watoto hao kwenye hospitali na kwenye mitandao ya kijamii kwamba watoto hao wachanga walikuwa wameachwa peke yao, akisema mkunga na muuguzi walikuwepo Jumatano jioni.