Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Januari 28, 2023 Local time: 13:40

Waziri wa Afya Senegal afukuzwa kazi


Waziri wa Afya Senegal afukuzwa kazi
please wait

No media source currently available

0:00 0:01:13 0:00

Rais wa Senegal Macky Sall Alhamisi amemfuta kazi waziri wake wa afya, Abdoulaye Diouf Zarr, amri ya serikali imeonyesha, baada ya watoto wachanga 11 kuuawa na moto katika chumba cha hospitali cha watoto wachanga.

Nafasi ya Sarr itachukuliwa na Marie Khemesse Ngom Ndiaye, mkurugenzi mkuu wa wizara ya afya, kwa mujibu wa amri hiyo ya serikali.

Maafisa wanasema hitilafu ya umeme ndio ilisababisha moto kuzuka Jumatano jioni na kuua watoto hao wachanga katika hospitali ya mji wa magharibi mwa Senegal wa Tivaouane.

XS
SM
MD
LG