Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 08, 2022 Local time: 18:54

Waziri Siraji auawa Mogadishu


Marehemu Abbas Abdullahi Sheikh Siraji.

Aliyekuwa Waziri wa Masuala ya Jamii na Kazi, Abbas Abdulahi Sheikh Siraji, 31, ameuawa mjini Mogadishu, Somalia.

Waziri mwenye umri mdogo katika serikali ya Somalia ameuawa kwa kupigwa risasi.

Abbas Abdulahi Sheikh Siraji, 31, alijizolea umaarufu mkubwa baada ya kushinda kiti cha ubunge kuwakilisha Jubbaland.

Japokuwa hakuwa ni mwenye uzoefu wa kisiasa alikabidhiwa wadhifa wa Waziri wa Masuala ya Kijamii na Kazi.

Siraji amewahi kuishi katika kambi ya wakimbizi ya Daadab nchini Kenya, lakini alirejea Somalia mwaka jana kushiriki uchaguzi mkuu na kushinda.

Kufuatia kifo chake, Rais wa nchi hiyo amekatiza kwa ghafla ziara yake ya Ethiopia ( Uhabeshi) na kurejea Somalia kuhudhuria mazishi yake.

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari Somalia saa chache kabla ya kuuawa alikuwa amezindua mradi wa ujenzi wa watumishi wa umma..

Aidha waziri wa habari wa Somalia amesema kuwa washukiwa wa mauaji hayo tayari wamekamatwa.

Imetayarishwa na mwandishi wetu Kennedy Wandera, Kenya

XS
SM
MD
LG