Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Aprili 21, 2025 Local time: 02:37

Waziri Rubio awasili Saudia kukutana na maafisa wa Ukraine


Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Marco Rubio akikutana na Mwanafalme wa Saudia Mohammed bin Salman, MaCHI 10, 2025. Picha ya Reuters
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Marco Rubio akikutana na Mwanafalme wa Saudia Mohammed bin Salman, MaCHI 10, 2025. Picha ya Reuters

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Marco Rubio Jumatatu alisema Marekani inatumai kutatua suala la misaada kwa Ukraine iliyositishwa katika mazungumzo ya Jumanne na maafisa wa Ukraine mjini Jeddah, Saudi Arabia.

Rubio amesema Marekani inatumia mbinu ya kusikiliza na inataka kufahamu ni kwenye masuala gani Ukraine iko tayari kulegeza msimamo.

“Waukraine tayari wanapata taarifa zote za ulinzi na kijajusi tunapozungumza hivi sasa. Nadhani suala la kusitisha misaada ni jambo ambalo natumai tunaweza kulitatua.

Bila shaka, yale yatakayotokea Jumanne yanagusia zaidi suala hilo,” Rubio aliwambia waandishi wa habari akiwa ndani ya ndege ya kijeshi kabla ya kutua Jeddah.

Baadaye Jumatatu, Mwanafalme wa Saudia Mohammed bin Salman alikutana na Rubio katika mji wa bandari wa Jeddah.

Salman alifanya mkutano tofauti na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky huko Riyadh mapema Jumatatu.

Leo Jumanne, Rubio ataungana na mshauri wa usalama wa taifa Mike Waltz kwenye mazungumzo ya Jeddah na maafisa wa Ukraine, huku Rais Donald Trump akishinikiza vita vya Ukraine vimalizike kwa haraka.

Forum

XS
SM
MD
LG