Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Juni 22, 2025 Local time: 11:43

Waziri mpya wa mambo ya nje wa China aanza ziara ya Afrika


Waziri mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed, akisalimiana na waziri mpya wa mambo ya nje wa China, Qin Gang, mjini Addis Ababa wakati akianza ziara ya Afrika, Januari 10, 2023. (Picha na AFP)
Waziri mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed, akisalimiana na waziri mpya wa mambo ya nje wa China, Qin Gang, mjini Addis Ababa wakati akianza ziara ya Afrika, Januari 10, 2023. (Picha na AFP)

Waziri mpya wa mambo ya nje wa China, Qin Gang, amewasili Ethiopia katika ziara yake ya kwanza barani Afrika, ambayo inajumuisha kuzitembelea  Gabon, Angola, Benin na Misri.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ethiopia na Naibu Waziri Mkuu Demeke Mekonnen, Jumanne asubuhi alimkaribisha mwenzake wa China kwenye kituo cha kwanza katika ziara yake ya mataifa matano barani Afrika.

Waziri wa Mambo ya Nje wa China, Qin Gang, yuko katika ziara yake ya kwanza barani Afrika tangu ateuliwe kufanya kazi hiyo mwezi Disemba baada ya kuhudumu tangu 2021 kama balozi nchini Marekani.

Baada ya kukutana na viongozi wa Ethiopia, Qin atatembelea makao makuu ya Umoja wa Afrika (AU) na Vituo vya Afrika vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (CDC) vilivyojengwa na China -vyote vikiwa na makao yake makuu mjini Addis Ababa.

CDC ya Kiafrika yenye thamani ya dola milioni 80 awali ilitazamwa kama ushirikiano wa Marekani, China na Afrika.

Lakini mpango huo uliporomoka chini ya utawala wa rais wa zamani wa Marekani, Donald Trump na kuwa mradi wa ushirika wa China na Umoja wa Afrika.

Marekani inaiona China kama mshindani wa kimkakati barani Afrika.

XS
SM
MD
LG