Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 28, 2023 Local time: 20:22

Waziri Mkuu wa zamani wa Malaysia Muhyiddin akamatwa, kukabiliwa na mshtaka kadhaa ya ufisadi


Waziri Mkuu wa zamani wa Malaysia akiwasili kuhojiwa na Tume ya Kupambana na Rushwa (MACC) mjini Putrajaya, Malaysia, March 9, 2023.

Malaysia siku ya Alhamisi imemkamata Waziri Mkuu wa zamani Muhyiddin Yassin na itamfungulia mashtaka ya ufisadi, taasisi ya kupambana na rushwa ya nchi hiyo imesema.

Tume ya Kupambana na Rushwa ya Malaysia (MACC) ilisema katika tamko lake Muhyiddin alikamatwa baada ya kuhojiwa kuhusu mradi wa kufufua uchumi ulioanzishwa na serikali yake.

Muhyiddin, ambaye alikuwa waziri mkuu kwa miezi 17 kati ya m waka 2020 na 2021, atafunguliwa mashtaka chini ya sheria inayohusu matumizi mabaya ya madaraka na utakatishaji fedha.

Waziri Mkuu huyo wa zamani na chama chake wanakabiliwa na uchunguzi dhidi ya ufisadi tangu Waziri Mkuu Anwar Ibrahim alipomshinda katika uchaguzi uliokuwa na ushindani mkali mwezi Novemba.

Anwar mwaka jana aliamuru tathminiifanyike kwa miradi ya serikali yenye thamani ya mabilioni ya dola iliyopitishwa na Muhyiddin ikiwemo miradi ya kuleta unafuu kwa athari za COVID-19, ikidaiwa haikufuata taratibu sahihi.

Muhyiddin awali amekanusha tuhuma hizo, akieleza kuwa ni kisasi cha kisiasa.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la Reuters.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG