Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 28, 2023 Local time: 21:05

Sierra Leone: Chama kikuu cha upinzani chamteua mgombea urais anaedaiwa kuiba pesa za umma dola milioni 2.5


Mgombea urais wa chama cha APC Samura Kamara wakati wa kampeni ya chama chake kaskazini mwa Sierra Leone, Machi 5, 2018

Chama kikuu cha upinzani nchini Sierra Leone, kimemteua waziri wa zamani wa mambo ya nje Samura Kamara kama mgombea wake wa urais licha ya uchunguzi dhidi yake kuwa anadaiwa kuiba dola milioni 2.5 ambazo ni pesa za umma.

Chama cha All People’s Congress ( APC) kimemchagua Kamara, ambaye alishindwa na Rais Julius Maada Bio katika uchaguzi uliopita, kama mgombea kwenye kinyang’anyiro cha urais mwezi Juni.

Kuteuliwa kwa Kamara kunajiri licha ya tangazo la Mahakama kuu kwamba uamuzi utatolewa Alhamisi juu ya kesi ya ufisadi dhidi yake na watu wengine watano.

Mwezi Disemba mwaka wa 2021, Kamara alishtakiwa kwa matumizi mabaya ya zaidi ya dola milioni 2.5 pesa za umma katika kesi iliyohusishwa na ukarabati wa ubalozi mdogo wa New York alipokuwa waziri wa mambo ya nje.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG