Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Julai 14, 2024 Local time: 13:01

Waziri mkuu wa Ujerumani akutana na Ramaphosa


Waziri mkuu wa Ujerumani na rais wa Afrika kusini Cyril Ramaphosa mapema leo
Waziri mkuu wa Ujerumani na rais wa Afrika kusini Cyril Ramaphosa mapema leo

Suala la Afrika kusini kutoegemea upande wowote kwenye vita vya Russia na Ukraine ni mojawapo wa masuala muhimu yaliokuwa kwenye mazunguzo kati ya chancela wa Ujerumani Olaf Scholz, na rais Cyril Ramaphosa wakati wa kukamilisha ziara za siku tatu nchini humo.

Akizungumza na wanahabari mjini Pretoria kabla ya kuanza mazungumzo yao ya faragha, viongozi hao pia walidokeza kuhusu baadhi ya matukio barani Afrika. Ziara ya Scholz imefanyika wakati vita vya Ukraine vikiendelea kwa takriban miezi mitatu na kusababisha kupanda kwa bei za mafuta na vyakula kote ulimwenguni likiwepo bara la Afrika.

Afrika kusini imekataa kuchukua msimo wowote na hasa kukemea Russia kutokana na uvamizi dhidi ya Ukraine na badala yake kuomba kufanyika kwa mazungumzo kati ya mataifa yote mawili. Scholz amesema kwamba ilikuwa ni muhimu kuzungumzia suala hilo na Ramaphosa.

Suala lingine muhimu kuzungumziwa ni viongozi hao ni kupunguza kutegemea makaa ya mawe kwenye baadhi ya viwanda nchini humo. Ujerumani ni moja ya mataifa yalioahidi hadi dola bilioni 8.5 wakati wa mkutano wa mazingira wa COP26 mwaka uliopita, ili kusaidia Afrika kusini kupunguza kutegemea nishati kutokana na makaa ya mawe.

Kufikia sasa bado hakujatolewa tamko lolote kuhusiana na fedha hizo. Afrika kusini imekuwa ikishuhudia kupotea kwa huduma za umeme mara kwa mara katika miaka ya karibuni kutokana na viwanda vya makaa ya mawe kushindwa kuzalisha umeme wa kutosha.

Kiongozi huyo ameahidi kuisaidia nchi hiyo yenye uchumi mkubwa barani afrika kufanya mabadiliko kuelekea nishati mbadala.

Scholz aliwasili Afrika kusini baada ya kutembelea Senegal na Niger, ambako alieleza azima ya Ujerumani ya kukuza sekta ya gesi nchini Senegal pamoja na misaada ya fedha na kijeshi kwa Niger.

Mtayarishaji: Harrison Kamau

XS
SM
MD
LG