Sanchez na dazeni ya mawaziri wanatarajiwa kuwa na kikao leo hii pamoja na wajumbe wa ngazi ya juu wa serekali ya Morocco.
Wanatarajia kutia saini mikataba kadhaa ikijumuisha ya uwekezaji, pamoja na majadiliano kuhusiana na changamoto za wahamiaji vimesema vyanzo vya serekali ya Morocco.
Kabla ya ziara, waziri mkuu Sanchez alizungumza kwa njia ya simu na mfalme Mohamed wa sita, ambaye ametoa mwito kwake kuangazia namna mpya ya uhusiano baina ya Morocco na Uhispania, kwa mujibu wa taarifa iliyo tolewa na ofisi ya waziri mkuu wa Uhispania.
Alitembelea Uhispania, Aprili mwaka jana baada ya kipindi kirefu cha mgogoro wa kidiplomasia.
Facebook Forum