Maafisa wamesema waziri mkuu alituma barua ya kujiuzulu kwa rais. Waziri mkuu aliandika pia kwenye Twitter kuhusu kujizulu kwake mapema Jumatatu asubuhi.
Kujiuzulu kwa waziri mkuu kumejiri baada ya wafuasi wa chama tawala cha Sri Lanka (SLPP) kuwashambulia Jumatatu waandamanaji wanaoipinga serikali, nje ya afisi za rais mjini Colombo, na kujeruhi watu 200.
Polisi walifyatua gesi ya kutoa machozi na mizinga ya maji na kuweka amri ya kutoka nje usiku ambayo haijulikani lini muda wake utamalizika.
Waandamanaji waliwashtumu viongozi hao ndugu kutoshughulikia ipasavyo kudorora kwa uchumi, hali mbaya ya uchumi ambayo nchi hiyo haijawahi kushuhudia tangu ijipatie uhuru mwaka wa 1948.