Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Agosti 16, 2022 Local time: 02:01

Hatimaye Waziri Mkuu wa Lesotho ajiuzulu


Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Lesotho Thomas Thabane

Waziri mkuu wa Lesotho Thomas Thabane hatimaye alijiuzulu Jumanne baada ya shinikizo kubwa kutoka kwa viongozi waliotaka aondoke kutokana na tuhuma za kuhusika katika mauaji ya mkewe wa kwanza Lipolelo Thabane mnamo mwaka wa 2017.

Awali Thabane, mwenye umri wa miaka 80, alikuwa ameahidi kuondoka madarakani mwishoni mwa mwezi Julai lakini wapinzani kutoka chama chake cha All Basotho Convention wakafanya mkataba na chama kikubwa cha upinzani cha Democratic Congress wa kuunda serikali mpya ya muungano.

Hatua hiyo ilimwacha Thabane bila chaguo ila kujiuzulu kufuatia kura ya kutokuwa na imani naye.

KIKAO

Katibu binafsi wa mfalme Monehela Posholi alisema Jumanne kuwa baraza la mawaziri wakati likifanya kikao hapo Jumatatu lilimshauri mfalme Letsie wa 3 kumuapisha waziri wa fedha Moeketsi Majoro kuwa waziri mkuu baadaye siku ya Jumatano.

Thomas Thabane na mkewe wa sasa Maesaiah Thabane
Thomas Thabane na mkewe wa sasa Maesaiah Thabane

Thabane alikuwa waziri mkuu kuanzia 2012 hadi 2015 na kisha baadaye akachukua wadhifa huo tena kuanzia 2017 hadi jana Jumanne.

-Imetayarishwa na Harrison Kamau, VOA, Washington DC

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG