Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Oktoba 02, 2023 Local time: 21:49

Waziri mkuu wa Israel aahirisha utekelezaji wa mpango wa mabadiliko ya mfumo wa mahakama


Maandamano ya Waisraeli mjini Jerusalem baada ya waziri mkuu Benjamin Netanyahu kumfuta kazi waziri wa ulinzi ambaye anapinga mpango wa kufanyia mabadiliko mfumo wa mahakama, Machi 27, 2023

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu Jumatatu ameahirisha mpango wake wa kufanya mabadiliko kwenye mfumo wa mahakama kutokana na maandamano makubwa na mgomo wa kitaifa wa wafanyakazi wanaopinga mpango huo.

Netanyahu amesema ameagiza utekelezaji wa sheria hiyo yenye utata usitishwe kwa muda hadi kikao cha bunge cha msimu wa joto ili kutoa fursa kwa ajili ya mazungumzo ya kweli.

Mpango huo unapendekeza bunge liwe na udhibiti mkubwa wa mahakama, ikiwemo uteuzi wa majaji na haki ya kubatilisha maamuzi ambayo bunge haliyataki.

Akitangaza kuahirishwa kwa mpango huo, Netanyahu amesema, “ Kitu kimoja ambacho siko tayari kukubali, kuna watu wachache wenye itikadi kali ambao wako tayari kuisambaratisha nchi, kutupeleka kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe na kutoa wito wa kutohudumu katika jeshi, jambo ambalo ni uhalifu mbaya.”

Kabla ya tangazo la Netanyahu, wafanyakazi wa Israel walianzisha mgomo wa kitaifa Jumatatu, na maelfu ya watu waliandamana tena nje ya bunge.

XS
SM
MD
LG