Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Juni 16, 2024 Local time: 05:34

Waziri Mkuu wa India anakwenda Afrika


Waziri Mkuu wa India, Narendra Modi atatembelea mataifa kadhaa ya Afrika wiki hii.
Waziri Mkuu wa India, Narendra Modi atatembelea mataifa kadhaa ya Afrika wiki hii.

Waziri Mkuu wa India Narendra Modi anaelekea Afrika Alhamis kuimarisha ushirikiano wa nchi yake na bara hilo lenye utajiri wa rasiliamali linaloonekana kama muhimu kwa usalama wa nishati na chakula kwa new Delhi.

Pia ataelezea India kama rafiki wa maendeleo kwa Afrika wakati ikitafuta kuondoa ushawishi mkubwa wa China katika eneo hilo. Ziara ya siku tano ya kiongozi huyo wa India inajumuisha Tanzania, Kenya, Afrika kusini na Msumbiji kufuatia mkutano mkubwa mjini New Delhi mwaka jana uliowashirikisha takribani wakuu wa mataifa 50 ya Afrika.

“Nchi zote hizi nne, ukiangalia ramani, ni majirani zetu wa baharini, wote ni milango kuelekea bara, nchi zilizozungukwa na ardhi ambazo ni marafiki muhimu, alisema Amar Sinha ambaye anashughulikia masuala ya ndani ya Afrika kwenye wizara ya mambo ya nje ya India. nishati na kilimo yatakuwa maeneo makuu ya kuongeza ushirikiano.

XS
SM
MD
LG