Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 07:39

Waziri Mkuu wa Ethiopia aunda kamati ya mashauriano kuzungumza na vikosi vya Tigray

Waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed.(REUTERS).
Waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed.(REUTERS).

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed alisema kwamba serikali kuu  imeunda kamati ya mashauriano kuzungumza na vikosi vya mkoa wa kaskazini wa  Tigray.

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed alisema kwamba serikali kuu imeunda kamati ya mashauriano kuzungumza na vikosi vya mkoa wa kaskazini wa Tigray.

Mapigano yalizuka huko Tigray Novemba 2020 na kusambaa katika mikoa jirani ya Afar na Amhara mwaka jana, lakini yamepungua tangu serikali kuu ilipotangaza kusitisha mapigano kwa ajili ya huduma za kibinadamu kwa upande wake mwezi Machi.

"Kuhusu amani, kamati imeanzishwa. Mashauriano yanahitaji kazi kubwa. Kamati imeundwa na itachunguza jinsi tutakavyofanya mazungumzo," Abiy aliliambia bunge.

Ni mara ya kwanza kwa Abiy kuweka hadharani taarifa kuhusu kamati hiyo.

Alisema Naibu Waziri Mkuu, Demeke Mekonnen ambaye ndiye anayeongoza kamati hiyo, ambayo itakuwa na siku 10 hadi 15 kufanyia kazi maelezo zaidi yatakayojadiliwa.

XS
SM
MD
LG