Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Julai 14, 2024 Local time: 22:07

Waziri mkuu wa Canada kukabiliwa na maswali lukuki juu ya ufadhili wa NATO


Waziri Mkuu wa Canada, Justin Trudeau
Waziri Mkuu wa Canada, Justin Trudeau

Waziri mkuu wa Canada, Justin Trudeau, anatarajiwa kukabiliana na maswali magumu katika mkutano wa wiki hii wa NATO, wa hapa Washington, kuhusu taifa lake kushindwa kufikia fungu la fedha zilizo afikiwa za ulinzi ikiwa ni sawa na asilimia mbili ya pato lake la taifa.

Mmoja wa wanachama 12 wa ushirika huo, Canada imekuwa ni mwanachama anayetumia fedha kidogo zaidi hata pale wengine walipoongeza matumizi yao wakati wa msukumo wa Marekani, na kukuwa tishio la Russia barani Ulaya.

Licha ya mwaka 2014 kuahidi kuongeza kufikia asilimia mbili, taifa hilo kwa sasa linatumia asilimia 1.34, likiwa linawashinda wanachama watano tu kwa matumizi hayo.

Mwezi Aprili, nchi hiyo ilitangaza mipango ya kuongeza kiasi hicho na kufikia asilimia 1.76 itakapofika bajeti ya mwaka 2029-2030.

Gazeti la The Washington Post mwezi uliopita liliripoti kwamba Canada imeipatia Ukraine zaidi ya dola bilioni moja za msaada wa kijeshi tangu kuzuka kwa vita dhidi ya Russia, Febuari 2022.

Forum

XS
SM
MD
LG