Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Juni 05, 2023 Local time: 12:23

Waziri Mkuu Somalia ajiuzulu


Waziri Mkuu wa Somalia Omar Abdirashid Ali Sharmake ajiuzulu baada ya mvutano mrefu na Rais Sharrif.

Rais wa Somalia Sheikh Sharrif Sheikh Ahmed anasema atafanya uteuzi wa waziri mkuu mpya hivi karibuni baada ya Waziri Mkuu Omar Abdirashid Ali Sharmake kujiuzulu leo na kumaliza mzozo wa muda mrefu kati yake na Rais Sharrif.

Bw.Sharmake alitangaza kujiuzulu Jumanne huko Mogadishu akiwa kando ya Rais Sharrif. Bw.Sharmake alisema amejiuzulu kutokana na mzozo wa kisiasa na kutokuwa na usalama Somalia.

Mawaziri wa serikali wamesema wanategemea kuwa serikali ijayo itaweza kuleta uthabiti nchini humo. Lakini wachambuzi wa Somalia wana wasi wasi wakisema kuwa uasi wa wanamgambo wa kiislam na mfumo wa kisiasa ulio dhaifu unafanya vigumu kwa serikali yeyote kuweza kufanya kazi.

XS
SM
MD
LG