Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Mei 26, 2024 Local time: 12:57

Waziri Mkuu Libya asema serikali yake inaunga mkono kuondolewa vikosi vyote vya kigeni

 Fathi Bashagha wa Libya, ambaye aliteuliwa kuwa waziri mkuu na bunge lenye makao yake mashariki mwa nchi hiyo akizungumza wakati wa mahojiano na Reuters mjini Tunis,
(March 30, 2022. REUTERS/Jihed Abidellaoui).
Fathi Bashagha wa Libya, ambaye aliteuliwa kuwa waziri mkuu na bunge lenye makao yake mashariki mwa nchi hiyo akizungumza wakati wa mahojiano na Reuters mjini Tunis, (March 30, 2022. REUTERS/Jihed Abidellaoui).

Waziri Mkuu aliyeteuliwa na bunge la Libya Fathi Bashagha alisema Jumatano kwamba serikali yake inaunga mkono kuondolewa kwa vikosi vyote vya kigeni na mamluki kutoka Libya, ikiongozwa na kamati iliyoundwa kulinda usitishaji vita baada ya mzozo wa 2014-2020.

Katika mahojiano na shirika la habari la Reuters mjini London, ambapo Bashagha anajaribu kutafuta uungwaji mkono kwa serikali yake kuchukua hatamu mjini Tripoli, kiongozi huyo alisema alikuwa mfuasi mkubwa wa kamati ya 5+5 ambayo ilikubali wapiganaji wa kigeni wafukuzwe.

Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 59 alisema serikali yake katika mji wa mashariki wa Sirte imeanza kazi yake licha ya Abdulhamid al-Dbeibah, ambaye alitawazwa kuwa waziri mkuu mwaka jana kupitia mchakato unaoungwa mkono na Umoja wa Mataifa, kukataa hatua yake, na kusababisha mzozo.

XS
SM
MD
LG