Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu walitoa wito kwa nchi mbalimbali duniani kulaani mashambulizi ya kushtukiza ya kundi la Hamas, wakisema huu ni wakati wa uwazi wa kimaadili.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Tel Aviv siku ya Alhamisi, Netanyahu alimshukuru Blinken kwa kufika Israel katikati ya mzozo huo na kwa msaada wa Marekani, huku akitoa maelezo yenye hisia kuhusu mashambulizi ambayo yameua zaidi ya Waisraeli 1,000.
Kuchomwa kwa watu wakiwa hai, kukatwa vichwa, kutekwa nyara kwa mvulana mdogo sio tu kutekwa nyara, kunyanyaswa, kuumiza, lakini shambulizi na maonyesho ya kuhuzunisha ya kusherehekea mambo haya ya kutisha, kusheherekea kutukuzwa kwa uovu. Rais Biden alikuwa sahihi kabisa kwa kuita huu ni uovu mkubwa, Netanyahu alisema.
Forum