Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Juni 20, 2024 Local time: 14:28

Wazazi waunga mkono hatua ya serikali kufuta shule za bweni Tanzania


Watoto nchini Tanzania wakisajili mbwa wao ili wapatiwe chanjo ya kichaa cha mbwa. Picha na Dk. Guy Palmer.
Watoto nchini Tanzania wakisajili mbwa wao ili wapatiwe chanjo ya kichaa cha mbwa. Picha na Dk. Guy Palmer.

Hatua ya serikali ya Tanzania kufuta shule za bweni kwa watoto kuanzia chekechea hadi darasa la nne imeungwa mkono na watanzania wengi wakielezea wameisubiria hatua hii kwa muda mrefu hatimaye imefika.

Kwa mujibu wa taarifa ya serikali hatua hii itaanza kutumika rasmi kuanzia Machi 31 mwaka huu.

Katika mahojiano na Sauti ya Amerika, baadhi ya wazazi wamesema shule za bweni zinawanyima watoto hao haki zao za msingi za kuwa karibu na wazazi au walezi wao.

Wamesema katika umri huo mdogo ambao ni muhimu katika maendeleo yao kimaisha na kutoa malezi ya msingi ya kujenga maadili ya watoto kiimani, kinidhamu, uwajibikaji na mahusiano na familia.

Daniel Marandu mkazi wa Dar es Salaam amesema shule za bweni zinaathiri mahusiano kati ya wanafunzi na wazazi wao, “badala ya mtoto kuwa karibu na mzazi, anakuwa karibu na mwalimu kwa hiyo mtoto anakuwa na maadili tofauti na yale ya mzazi anayotaka”

Kwa mujibu wa gazeti la The East African kamishina wa wizara ya elimu Dk. Lyabwene Mtahabwa alisema kuwapeleka watoto wadogo katika shule hizo kunawakosesha msingi wa malezi na makuzi yanayofanywa na familia ambao ni wazazi au walezi wao.

"Kutokana na utafiti wetu, shule nyingi zinalenga katika kuhakikisha wanafunzi wanafaulu mitihani yao, na miongoni mwa mikakati inayotumika ni kuanzisha shule za bweni na kambi za kitaaluma zinazoendeshwa wakati wa likizo, na hiyo inasababisha udhaifu katika juhudi za kuijenga tabia ya wanafunzi," alisema Dk. Mtahabwa.

Wizara ilisema itakuwa ikifanya ukaguzi wa ghafla mashuleni, na shule yoyote itakayobainika kukiuka maagizo hayo itachukuliwa hatua za kinidhamu, kisheria au kufutiwa usajili.

XS
SM
MD
LG