Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 10:46

wazanzibari watofautiana juu ya tathmini ya Warioba


Russian President Vladimir Putin, center, takes part in a wreath-laying ceremony at the Tomb of the Unknown Soldier outside Moscow's Kremlin Wall.
Russian President Vladimir Putin, center, takes part in a wreath-laying ceremony at the Tomb of the Unknown Soldier outside Moscow's Kremlin Wall.
Baadhi ya wananchi, wasomi na wanasiasa huko visiwani Zanzibar wamesema muundo wa Serikali tatu uliopendekezwa katika rasimu ya pili ya katiba utachangia kuudhofisha Muungano wa Tanzania na kuondokana na uzalendo uliodumu na kuimarika kwa miaka 50 tangu kuasisiwa kwake na hayati Mwalimu Julius kambarage Nyerere na marehemu Sheikh Abeid Amani Karume.

please wait

No media source currently available

0:00 0:02:07 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Mara baada ya kuwasilishwa kwa rasimu ya pili ya katiba katika bunge maalum la katiba, huko visiwani Zanzibar kumekuwepo na gumzo kubwa kuhusu mapendekezo yaliyomo kwenye rasimu hiyo, ambapo pia biashara ya CD zenye hotuba na masuala ya rasimu ya katiba zinauzwa kwa wingi katika soko kuu la Darajani.

Wakizungumza katika mahojiano maalum baadhi ya wasomi na wanasiasa wamesema mfumo wa serikali mbili ulipaswa kufanyiwa marekebisho na kutatua changamoto pamoja na kero zote za muungano, badala ya kuanzisha utaratibu mpya wa kuwa na serikali tatu ambao unaweza kudhoofisha Muungano.

Miongoni mwa waliotoa maoni yao ni pamoja na mwanasheria mkongwe hapa nchini Hamid Mbwezeleni, pamoja na baadhi ya wanasiasa na wananchi ambao wamesema kuwa muungano wa serikali mbili ndio unaofaa kuendelea kutumika kwa vile umeijengea heshima Tanzania na kuwa mfano bora mbele ya jumuiya ya kimataifa kwa kuwa na Muungano uliodumu kwa miaka 50.
XS
SM
MD
LG