Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Septemba 27, 2022 Local time: 10:58

Uchaguzi mkuu wenye ushindani mkali wafanyika Zambia


Wafuasi wa Rais Edgar Lungu, kiongozi wa chama cha Patriotic Front party (PF), wakusanyika mjini Lusaka,siku moja kabla ya uchaguzi mkuu, Aug. 10, 2016.

Chama tawala cha Zambia Patriotic Front kinakabiliwa na upinzani mubwa katika uchaguzi wa rais siku ya Alhamisi. Rais Edgar Lungu aliyechaguliwa baada ya kifo cha aliyemtangulia anakabiliwa na mashindano na mpinzani wake mkuu, aliyemshinda kwa idadi ndogo kabisa ya kura miaka miwili iliyopita Hakainde Hichilema.

Tangu ushindi huo taifa hilo limekumbwa na ukame, upungufu wa chakula, mvutano mkubwa wa kisiasa na matatizo mengine ya kiuchumi.

FILE - Mgombea wa upinzani Hakainde Hichilema awahutubia wafuasi wake mjini Lusaka, Zambia.
FILE - Mgombea wa upinzani Hakainde Hichilema awahutubia wafuasi wake mjini Lusaka, Zambia.

Uchaguzi mkuu unagubikwa na wasi wasi wa uwezekano wa kuzuka ghasia pale rais Lungu akikabiliwa na ushindani mkali kutoka kiongozi wa upinzani Hichilema wa chama cha UPND.

Lungu anaechukulia mashuhuri miongoni mwa wananchi wa Zambia alimshinda kwa kura chache Hichilema mfanya biashara wakati wa uchaguzi wa mapema uloitishwa Januari 2015 kufuatia kifo cha ghafla cha rais Michael Sata.

FILE - Rais Edgar Lungu akihutubia maelfu ya wafuasi wake May 21, 2016, akizindua kampeni yake ya uchaguzi.
FILE - Rais Edgar Lungu akihutubia maelfu ya wafuasi wake May 21, 2016, akizindua kampeni yake ya uchaguzi.

Uchaguzi wa mwaka huu umegubikwa na mapambano kati ya wafuasi wa vyama viwili vikuu, na kumsababisha mkuu wa tume ya uchaguzi kusema ghasia ni jambo lisilo la kawaida wakati wa uchaguzi nchini humo.

Zambia inasififiwa kama nchi moja wapo ya kusini mwa afrika iliyootesha mizizi ya kidemokrasia na amani.

Wachambuzi wanasema ni vigumu hadi hii leo kusema nani ataweza kushinda lakini wote wanatabiri uwezekano wa kutokea ghasia.

Kiongozi aliyemtangulia Lungu, Gary Scott, aliyekua makamu rais wa Sata hana uhusiano wala urafiki na Lungu, na hivi karibuni amemunga mkono Hichilema.

Mwanasiasa huyo mkongwe anasema anapigwa na butwa kuona jinsi taifa hilo linalosifiwa kwa utulivu na amani kutumbukia katika hali ya ghasia. Anasema tatizo kuu ni usimamizi mbaya wa uchumi na uwongozi dhaifu.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG