Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 13, 2024 Local time: 07:06

Wazambia wajiandaa na upigaji kura jumanne


Kaimu Rais wa Zambia, Guy Scott.
Kaimu Rais wa Zambia, Guy Scott.

Ofisa mmoja mwandamizi wa tume ya uchaguzi nchini Zambia anasema tume ipo tayari kusimamia uchaguzi wa rais wenye hadhi unaotarajiwa kufanyika jumanne. Kampeni rasmi zinaisha jumatatu kabla ya upigaji kura.

Mkurugenzi wa tume ya uchaguzi bibi Priscilla Isaac alisema vifaa vyote muhimu na visivyo muhimu vilishapelekwa kwenye vituo kuhakikisha vituo vyote vya kupiga kura nchi nzima vinaweza kufunguliwa kwa wakati kwa ajili ya upigaji kura. Alisema vyama vya siasa vilikuwa sehemu ya utaratibu wa kuthibitisha karatasi za kupiga kura na kwamba vyama vilionekana kuridhishwa na utaratibu mzima.

Baadhi ya wazambia wanaelezea wasi wasi kuhusu ghasia baada ya wafuasi kutoka chama tawala cha Patriotic Front na upinzani wa chama cha United Party for National Development kupambana katika maeneo ya nchi kati kati ya kampeni zao.

XS
SM
MD
LG