Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 29, 2023 Local time: 23:35

Wawili wauwawa kwa kupigwa risasi katika siku ya tano ya maandamano katika mji wa Cape Town


Waandamanaji wakikimbia huku mabomu ya machozi yakirushwa wakati wa mgomo unaoendelea wa wahudumu wa teksi dhidi ya mamlaka ya trafiki mjini Cape Town, Afrika Kusini, Agosti 7, 2023 REUTERS.

Polisi wanasema mtu mmoja aliuwawa na wengine watatu kujeruhiwa kwa risasi Jumatatu karibu na uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Cape Town

Watu wawili wameuwawa kwa kupigwa risasi katika siku ya tano ya maandamano ya ghasia katika mji wa Cape Town nchini Afrika Kusini yaliyosababishwa na mzozo wiki iliyopita kati ya madereva wa mabasi madogo na mamlaka.

Polisi wanasema mtu mmoja aliuwawa na wengine watatu kujeruhiwa kwa risasi Jumatatu karibu na uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Cape Town baada ya waandamanaji kulipiga gari kwa mawe na dereva akajibu kwa kuwafyatulia risasi. Mtu mmoja alifariki dunia kwa majeraha mengi ya risasi katika shambulizi risasi tofauti.

Ukamataji huo katika kwenye viunga vya mji wa pili kwa ukubwa Afrika Kusini yanafuatia tangazo la Alhamisi iliyopita la mgomo wa wiki moja wa madereva wa mabasi madogo waliokasirishwa na kile wanachokiita mbinu nzito za polisi na mamlaka ya jiji.

Forum

XS
SM
MD
LG