Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Februari 25, 2024 Local time: 11:29

Wawili wakamatwa kuhusiana na mauaji ya Nemtsov


Picha ya Boris Nemstov na maua katika eneo alilouliwa karibu na bunge la Russia (Kremlin).
Picha ya Boris Nemstov na maua katika eneo alilouliwa karibu na bunge la Russia (Kremlin).

Russia imewakamata na kuwazuilia watuhumiwa wawili wanaohusishwa na mauaji wa kiongozi wa upinzani Boris Nemtsov.

Mkuu wa idara ya ulinzi katika serikali kuu Alexander Bortnikov aliiambia televisheni rasmi ya Russia Jumamosi kuwa wanaume hao wawili Anzor Gubashev na Zaur Dadayev kutoka eneo lenye msukosuko la kaskazini mwa Russia wanatuhumiwa kwa mauaji hayo.

Mauaji ya Februari 27 ya kiongozi huyo mashuhuri na mkosaji mkali wa serikali, karibu na Kremlin, yalitikisa nchi hiyo. Wanachama wa upinzani wanatupia lawama serikali wakisema Nemtsov aliuawa kulipiza kisasi shtuma zake kali dhidi ya rais wa Russia Vladmir Putin.

Mshirika wa karibu wa Nemtsov katika upinzani, Ilya Yashin, alieleza mashaka juu ya watuhumiwa hao kupitia Facebook akisema ni vigumu sana kubaini ikiwa wao ndiyo wauwaji na kuongeza kwamba waliomrisha Nemtsov auawe wanapaswa kutambulishwa.

XS
SM
MD
LG