Boti ya Esther Miracle ilikuwa katika safari ya usiku kutoka mji mkuu Libreville kwenda mji wa bandari wa Port-Gentil ikiwa na abiria 151 ndani yake wamesema maafisa wa bandari walozungumza na AFP.
Kupitia ujumbe wa Facebook, kampuni ya Royal Coast Marine ambayo inamiliki boti hiyo imesema kati ya saa tisa na kumi Alfajiri kulitokea mawimbi ambayo yalisababisha boti hiyo kupoteza mwelekeo wake.
Naibu waziri wa usafirishaji, Eric Joel Bekele alitoa video katika ukurasa wa Facebook akisema boti hiyo imezama majira ya saa tisa na dakika 58 katika mwambao wa Libreville na watu 121 wameokolewa lakini kwa masikitika watu wawili wamefariki dunia huku mamlaka zinazo husika zikianzisha uchunguzi.
Aafisa wa bandari ambaye amezungumza kwa masharti ya kutotajwa amesema watu 28 hawajulikani walipo.
Facebook Forum