Boti hiyo iliondoka katika mji mkuu, Jakarta, Machi 3 ikielekea katika kisiwa cha Lombok, ikiwa imebeba tani za samaki na vifaa ilipokumbwa na dhoruba na mawimbi makubwa katikati ya safari Jumamosi katika sehemu ya bahari ya jimbo la Sulawesi Kusini.
Wavuvi hao 11 wakiwa wamevalia jaketi za kuokoa maisha, walipotea kwa siku kadhaa mpaka walipoonwa na wavuvi wa eneo hilo kwenye visiwa vya mbali vya Selayar katika jimbo la Sulawesi Kusini.
Miili ya wafanyakazi wengine wawili pia iligunduliwa katika eneo hilo. Ajali za baharini hutokea mara kwa mara Indonesia, yenye visiwa 17,000 na raia milioni 270.
Forum