Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 22, 2024 Local time: 17:59

23 wauwawa katika mapigano kati ya wakulima na wafugaji Nigeria


Mkulima akipukuta maganda ya mpunga katika shamba lake huko Benue, Nigeria Desemba 3, 2019. REUTERS.
Mkulima akipukuta maganda ya mpunga katika shamba lake huko Benue, Nigeria Desemba 3, 2019. REUTERS.

Mapigano kati ya wafugaji na wakulima katika jimbo la Benue nchini Nigeria yalisababisha vifo vya takriban watu 23, afisa mmoja wa eneo hilo alisema siku ya Alhamisi.

Tukio la hivi karibuni lililochochewa na shinikizo la kuongezeka kwa rasilimali za ardhi katika nchi hiyo yenye watu wengi zaidi barani Afrika.

Vurugu kati ya wakulima na wafugaji zimezidi kuwa jambo la kawaida katika miaka ya hivi karibuni huku ongezeko la watu likisababisha upanuzi wa eneo lililopangiwa kwa kilimo, na kuacha ardhi ndogo inayopatikana kwa malisho ya wazi na mifugo ya wahamaji.

Kertyo Tyounbur, mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Ukum eneo la Benue ambako ghasia zilitokea, alitoa idadi ya waliofariki kuwa 23.

Mkazi wa eneo hilo William Samson alisema shida ilianza Jumanne wakati wanakijiji waliwaua wafugaji wawili na kuiba ng'ombe wao. Hii ilifuatiwa na mashambulizi ya kulipiza kisasi ya wafugaji siku ya Jumatano kwenye kijiji cha Gbeji, alisema.

Reuters haikuweza kuthibitisha maelezo yake kutoka kwa vyanzo vingine katika eneo la kijijini.

XS
SM
MD
LG