Shambulizi la mchana katikati mwa Peshawar, mji mkuu wa jimbo la Pakhtunkhwa, lilifanywa nje na mjitoa muhanga kwa mujibu wa polisi.
Afisa wa juu wa polisi wa Peshawar aliithibitishia kwa VOA idadi ya wote waliofariki dunia, inaweza kuongezeka na bado kuna waumini ambao bado hawaja hesabiwa na miili haijatambuliwa.
Afisa wa juu wa usalama, naibu kamishina Shafiullah Khan, amesema watu wawili walio nusurika walikutwa katika kifusi.
Maafisa wa hospitali wa mji walithibitisha kupokea dazeni ya walio jeruhiwa, na kuelezea hali zao kuwa ni mbaya. Walio athirika wengi wao waliokuwa ni polisi wa jimbo.
Facebook Forum