Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Aprili 14, 2024 Local time: 23:15

Waumini washambuliwa kwa mabomu Nigeria


Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan (akiwa katika eneo la jengo la gazeti la "ThisDay" lililoshambuliwa kwa bomu April 26
Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan (akiwa katika eneo la jengo la gazeti la "ThisDay" lililoshambuliwa kwa bomu April 26

Maafisa wa usalama wanasema watu hao waliokuwa na silaha walikuwa wanaendesha pikipiki wakati walipofanya shambulizi hilo


Mashahidi kaskazini mwa Nigeria wanasema washambuliaji walirusha mabomu yaliyotengeneza nyumbani kwa waumini wakati wa ibada ya kikristo na baadae kufyatua risasi walipokuwa wakikimbia na kuuwa watu 15.

Maafisa wa usalama wanasema watu hao waliokuwa na silaha walikuwa wanaendesha pikipiki wakati walipofanya shambulizi hilo kwenye chuo kikuu cha Kano wakati ibada ikiendelea jumapili.

Maafisa wanasema washambuliaji walitoroka kabla ya maafisa wa usalama kuwasili hivyo kuwalazimu polisi kulifunga eneo hilo na kuwazuia hata maafisa wa afya kwa muda .

Maafisa wa usalama wanasema watu hao waliokuwa na silaha walikuwa wanaendesha pikipiki wakati walipofanya shambulizi hilo katika chuo cha Kano wakati ibada ikiendelea.

hakuna aliyedai kuhusika na shambulizi hilo, ambalo linafuatiwa na madai kama hayo yanayodhaniwa kufanywa na kundi lenye msimamo mkali la boko haram.


Kundi hilo limedai kufanya mashambulizi ya mauaji alhamisi katika ofisi za gazeti la “ this day “ katika mji wa kaskazini wa kaduna na mji mkuu Abuja.

XS
SM
MD
LG