Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Februari 09, 2023 Local time: 01:35

Watu 15 wauawa katika mapambano Somalia - ripoti


Map of Somalia

Maafisa wa Somalia wanasema watu 15 wameuwawa wakati wa siku mbili za mapambano katika kijiji kimoja huko kusini-magharibi mwa nchi hiyo. Kundi la Al-Shabaab lilishambulia kituo katika kijiji cha Moragabey kwenye jimbo la Bokol lililotumiwa na majeshi ya kieneo ya serikali jana Jumatatu, lakini mapambano yaliendelea hadi siku iliyofuata, kwa mujibu wa maafisa.

Vyanzo vya karibu na jeshi la Somalia viliiambia Sauti ya Amerika kwamba wanajeshi wanane wa kieneo na wanamgambo saba ni miongoni mwa waliokufa. Vyombo vya habari vinavyounga mkono kundi la Al-Shabaab viliripoti kwamba kijiji kilitekwa na wapiganaji wao jana jumatatu lakini Mohamed Moalim Ahmed, meya wa mji wa karibu na Huddur, na wakazi wa eneo hilo walikanusha madai haya.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG