Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 01:20

Watuhumiwa wa ubakaji na matumizi mabaya ya mitandaoni wakamatwa Tanzania


Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto nchini Tanzania, Ummy Mwalimu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto nchini Tanzania, Ummy Mwalimu

Habari hizo zilitanda katika mitandao ya kijamii tangu kutokea kwa tukio hilo Aprili 4 huku wamiliki wa mablogu na wanasiasa nchini Tanzania wakilaani kitendo hicho kama udhalilishaji wa kijinsia.

Polisi nchini Tanzania imewakamata watu 11 ikiwa ni pamoja na watuhumiwa wawili wakuu katika kesi iliyojumuisha ubakaji na matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii nchini humo. Kulingana na ripoti ya polisi watuhumiwa wakuu wawili Zuberi Thabiti (30) na Iddy Adamu (32) wamekamatwa kwa madai ya kumbaka msichana mwenye umri wa miaka 21 mkoani Morogoro na kurekodi tukio hilo katika simu na baadaye kusambaza katika mitandao ya kijamii.

Habari hizo zilitanda katika mitandao ya kijamii tangu kutokea kwa tukio hilo Aprili 4 huku wamiliki wa mablogu na wanasiasa nchini Tanzania wakilaani kitendo hicho kama udhalilishaji wa kijinsia.

Naye mkuu wa wilaya ya Mvomero ambako kitendo hicho kilitokea, Betty Mkwasa, Jumatatu aliandika katika mtandao wa Facebook akithibitisha kukamatwa kwa watuhumiwa hao na kuonya watu wengine kutosambaza kanda hiyo katika mitandao kwamba watashitakiwa kulingana na sheria za mitandao nchini humo.

Taarifa ya polisi imesema mtuhumiwa Zuberi Thabiti anayesemekana kuwa na uhusiano wa kimapenzi na msichana huyo alimwita katika nyumba ya wageni na kumruhusu mtuhumiwa wa pili Iddy Adamu kumbaka msichana huyo huku wakipiga picha za video kwa kutumia simu.

Watuhumiwa wengine tisa wametiwa hatiani kwa kupokea kanda hiyo na kuisambaza katika mitandao ya kijamii kinyume na sheria mitandao ya kijamii nchini Tanzania.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto nchini Tanzania, Ummy Mwalimu, Jumatatu alitumia nafasi yake bungeni na kukemea suala hilo na kutaka watuhumiwa wafikishwe mbele ya sheria.

Tukio hilo limekuwa suala kubwa katika mitandao ya kijamii Tanzania ambamo wamiliki na watu wengine wengi wamekemea kitendo alichofanyiwa msichana huyo, na pia uenezaji wa kanda katika mitandao ya kijamii.

XS
SM
MD
LG