Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Aprili 15, 2024 Local time: 03:37

Watuhumiwa wa Kenya wafikishwa ICC.


Mwendesha mashitaka mkuu wa ICC Luis Moreno Ocampo.
Mwendesha mashitaka mkuu wa ICC Luis Moreno Ocampo.

Bw. William Rutto, waziri wa zamani wa viwanda Henry Kosgei na mtangazaji wa radio Joshua Sang watafikishwa mahakamani saa nne na nusu asubuhi saa za Kenya.

Safari ya kwenda The Hague kwa watuhumiwa 6 wa ghasia za baada ya uchaguzi nchini Kenya imeanza Alhamisi wakati watatu kati ya washukiwa sita watakapofika mbele ya mahakama ya ICC.

Waziri aliyesimamishwa kazi William Rutto, waziri wa zamani wa viwanda Henry Kosgei na mtangazaji wa radio Joshua Sang watafikishwa mahakamani saa nne na nusu asubuhi saa za Kenya.

Watakuwa na kikao kifupi ambapo majaji hao watawatambua washukiwa na kuwasomea kila mmoja mashitaka na kuwajulisha haki zao kama mkataba wa Roma unavyosema ambao ulianzisha mahakama hiyo.

Bw. Ruto , Bw. Kosgey na Bw. Sang hawatatakiwa kujibu wala kukanusha mashitaka dhidi yao wakati wa kutajwa kwa kesi hiyo kwenye mahakama.

Na siku ya Ijumaa itakuwa ni zamu ya naibu waziri mkuu Uhuru Kenyatta, mkuu wa utumishi wa umma Francis Muthaura na mkuu wa zamani wa Polisi Hussein Ali kusimama kizimbani kwenye mahakama hiyo saa kumi na nusu jioni saa za Kenya.

XS
SM
MD
LG