Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 10:00

Watu zaidi ya 60 wafa Kenya baada ya bomba la mafuta kulipuka


Wakazi wa kitongoji cha Sinai, wakiwatizama wazima moto wakijaribu kuzima moto kufuatia mripuko kwenye bomba la mafuta karibu na Nairobi, Kenya Jumatatu Septemba 12, 2011
Wakazi wa kitongoji cha Sinai, wakiwatizama wazima moto wakijaribu kuzima moto kufuatia mripuko kwenye bomba la mafuta karibu na Nairobi, Kenya Jumatatu Septemba 12, 2011

Polisi wa mjini Nairobi wanasema miili ya watu 61 imepatikana mpaka sasa lakini wanatarajia idadi ya vifo kuongezeka.

Mashahidi katika mji mkuu wa Kenya , Nairobi wanasema dazani za watu wameuwawa na mlipuko baada ya bomba la mafuta kulipuka.

Polisi wa mjini Nairobi wanasema zaidi ya watu 100 huwenda wamefariki na wanatarajia idadi ya vifo kuongezeka.

Zaidi ya waathiriwa 100 walioungua moto walipelekwa katika hospitali za ndani baada ya bomba hilo la mafuta kulipuka jumatatu katika eneo lenye watu wengi la Sinai.

Mlipuko huo ulisababisha miili ya watu kuzagaa katika mitaa ambako watu wengi walikimbilia wakijaribu kuzima moto katika nguo zao na nywele zao.

Moto kutokana na mlipuko huo pia ulichoma baadhi ya majengo yaliyokuwa karibu .

Mashahidi wanasema bomba hilo la mafuta lililolipuka lilikuwa linavuja na watu walikuwa wanakwenda katika eneo lililoko kuchota mafuta. Polisi wanakisia kuwa moto wa sigara ndio uliosababisha mlipuko huo.

Matukio ya ajali kama hayo ni ya kawaida katika bara la afrika ambako mabomba ya mafuta yanavuja na magari makubwa ya kubeba mafuta yanapopata ajali vinashawishi kundi kubwa la watu kujaribu kuchota mafuta.

Mwaka 2009 takriban watu 120 waliuwawa magharibi mwa Kenya wakati gari kubwa na lafuta lilipopinduka na kuungua moto.

XS
SM
MD
LG